Ushauri Wa Engin Firat kwa FKF

SHIRIKISHO.
Kocha mpya anayeifunza timu ya taifa la Kenya Harambee stars,Mturuki Engin Firat ,alilishauri shirikisho la kandanda nchini humo Fkf likiongozwa na Rais Nick Mwendwa,kuboresha Miundo mbinu kama vile ujenzi Wa viwanja na elimu kwa makocha.
Engin wakati wake Wa kuzinduliwa rasmi,aliipa changamoto Fkf kwamba kama vijana wadogo hawatopata msingi sahihi,kutoka kwa makocha walioelimishwa ,basi itakuwa vigumu kuwafunza ukubwani.
MAKOCHA.
Kocha Firat ambaye anajiandaa kwa kibarua cha kuisaidia Stars kufuzu katika dimba la dunia Qatar 2022,aliwapa makocha nao changamoto ya kutotegemea kazi ya ukocha pekee kama kitega uchumi kwao.
KANDARASI.
Kuhusu kandarasi yake ya miezi miwili na stars,kocha huyu Wa zamani Wa Moldovia,alisema kuwa anataka kutathmini mazingira ya kazi kwanza na matokeo atakayotoa uwanjani. kocha Firat na Rais Wa Fkf Nick mwendwa.
Picha:Fkf media.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Maisha ya kutisha ya Eden Hazard.

The Unknown about Pep Quardiola.

Sergio Ramos afichua makubwa kuhusu Mbappe.