Wanachui AFC leopards wameduwaza mashabiki Wa ligi kuu nchini Kenya kwa kuichakaza Tusker united ambao ndio mabingwa Wa tetezi kichapo cha goli moja sifuri.
EDEN HAZARD. FAMILIA. Nyota huyu Wa kimataifa Wa ubelgiji amezaliwa kwao ubelgiji katika familia ya watoto 4 vijana dume wote na baba na mama. Kaka zake ni Ethan,Kylian na Thorgan. Baba na Mama walikuwa wachezaji Wa soka na hivyo kuifanya familia hiyo kuwa ya wanamichezo. Hakuna Dada. Hazard ,Thorgan na kylian walikua kwa pamoja wakipendana kwa kuendesha baiskeli na baba yao kuwabatiza the tripod . Hazard,kylian na Thorgan.Wakiwa wamevalia jezi nambari 10 ufaransa iliyovaliwa na Zidane wakati huo. Familia ya kina Hazard katika picha moja. WAZAZI. Thierry hazard alikuwa kiungo kati mlinzi naye mkewe carine Hazard alikuwa nyota wa kupigiwa mfano. Ba adhi ya vilabu alivyocheza babake Hazard. Stade Brainois Jul 1, 1998 AFC Tubize Jul 1, 1996 AA La Louviere Jul 1, 1991 Marchienne Ass. Jul 1, 1989 Stade Brainois until Jul 1, 1989 Mamake Carine,alicheza katika timu za ligi ya wanawake ubelgiji divisheni ya kwanza. Soma hii : Mamake Hazard alistaafu soka akiwa na...
Hatihati zimekuwepo nyingi kuhusu kusalia kwa winga Wa kifaransa kylian Mbappe katika timu ya PSG. Kabla ya dirisha la usajili kufungwa ,Real Madrid walikuwa karibu kumnasa katika dakika za jioni ila mabosi PSG wakagoma. SHINIKIZO LA MASHABIKI. Labda ukiwasikia wengi wananadi kwamba ni wakati mwafaka Wa Mbappe kuiacha PSG na kuenda kukiwasha laliga,jambo ambalo kwa wengine sio sawa, kwani anacheza nao nyota waliotoka hio laliga ,kina Lionel Messi na Neymar. JIBU. Sasa katika hili beki Sergio Ramos aliyegonga vichwa vya habari baada ya kuiacha Real Madrid na kujiunga na wakwasi hawa Wa Ufaransa Le Champione psg,wamesema haya nikimnukuu" Mbappe ana furaha sana akiwa hapa kinyume na Mashabiki wanavyotarajia.Kila wakati anazungumza na Messi na Neymar,wakijadili namna ya kujenga kikosi bora cha mashambulizi." Ramos huyo kaibua makubwa. Neymar kushoto,kati Mbappe na Messi kulia. Picha: Getty Author: Mwanamichezo blog E-mail: michezoh@gmail.com
SHIRIKISHO . Kocha mpya anayeifunza timu ya taifa la Kenya Harambee stars,Mturuki Engin Firat ,alilishauri shirikisho la kandanda nchini humo Fkf likiongozwa na Rais Nick Mwendwa,kuboresha Miundo mbinu kama vile ujenzi Wa viwanja na elimu kwa makocha. Engin wakati wake Wa kuzinduliwa rasmi,aliipa changamoto Fkf kwamba kama vijana wadogo hawatopata msingi sahihi,kutoka kwa makocha walioelimishwa ,basi itakuwa vigumu kuwafunza ukubwani. MAKOCHA. Kocha Firat ambaye anajiandaa kwa kibarua cha kuisaidia Stars kufuzu katika dimba la dunia Qatar 2022,aliwapa makocha nao changamoto ya kutotegemea kazi ya ukocha pekee kama kitega uchumi kwao. KANDARASI . Kuhusu kandarasi yake ya miezi miwili na stars,kocha huyu Wa zamani Wa Moldovia,alisema kuwa anataka kutathmini mazingira ya kazi kwanza na matokeo atakayotoa uwanjani. kocha Firat na Rais Wa Fkf Nick mwendwa. Picha:Fkf media.
Maoni
Chapisha Maoni