Maisha ya kutisha ya Eden Hazard.

EDEN HAZARD.
FAMILIA.
Nyota huyu Wa kimataifa Wa ubelgiji amezaliwa kwao ubelgiji katika familia ya watoto 4 vijana dume wote na baba na mama. Kaka zake ni Ethan,Kylian na Thorgan. Baba na Mama walikuwa wachezaji Wa soka na hivyo kuifanya familia hiyo kuwa ya wanamichezo. Hakuna Dada. Hazard ,Thorgan na kylian walikua kwa pamoja wakipendana kwa kuendesha baiskeli na baba yao kuwabatiza the tripod.
Hazard,kylian na Thorgan.Wakiwa wamevalia jezi nambari 10 ufaransa iliyovaliwa na Zidane wakati huo.Familia ya kina Hazard katika picha moja.

WAZAZI.
Thierry hazard alikuwa kiungo kati mlinzi naye mkewe carine Hazard alikuwa nyota wa kupigiwa mfano. 
Baadhi ya vilabu alivyocheza babake Hazard.
Stade Brainois
Jul 1, 1998
AFC Tubize
Jul 1, 1996
AA La Louviere
Jul 1, 1991
Marchienne Ass.
Jul 1, 1989
until Jul 1, 1989
Mamake Carine,alicheza katika timu za ligi ya wanawake ubelgiji divisheni ya kwanza.
Soma hii: Mamake Hazard alistaafu soka akiwa na ujauzito Wa Hazard Wa miezi 3. Kisha babake akastaafu mwaka 2001 mwezi julai.
Hazard pamoja na wazazi wake.kushoto carine mamake na kulia ni babake Thierry.

MAISHA YA HAZARD KISOKA.
Nyota huyu alikua kama mtoto Wa kawaida kwani familia yao ilikuwa ya wastani. Maisha ya soka alianzia katika Akademia ya timu ya Tubize ubelgiji kabla ya kuhamia ufaransa katika Akademia ya Lille. Aliibuka mwiba akiwa lille kilichowavutia Chelsea na kumnasa kwa uhamisho Wa £32milioni na baadaye kuenda Real Madrid kwa uhamisho Wa £100m.
Hazard akiitumikia lille.Hazard akisherehekea goli akiwa Chelsea.Hazard akiiitumikia Real Madrid

MAPENZI.
Kama binadamu mwingine tu Hazard alinasa penzi la mkewe Natacha van Honacker, akiwa na umri Wa miaka 14 wakiwa ubelgiji, wakati huo Hazard akichezea Akademia ya Tubize club.
Hazard alipoondoka nyumbani kuenda ufaransa ,hali ikawa ngumu kwa penzi lao kwa sababu ya Umbali. Penzi halina mipaka,kichuna alikuwa keshadata kwa penzi la Gwiji huyu Wa chenga. Natacha aliendelea na masomo kisha akaondoka nyumbani mwaka 2012 akiwa na miaka 18 kujiunga na mpenziwe Hazard Ufaransa,walipofunga pingu za Maisha.
Mkewe Hazard.

WATOTO.
Hazard na Natacha wana watoto watatu. Yannis ambaye alizaliwa kabla yao kuoana katika mishe za kutembeleana mwaka 2019 mwezi disemba tarehe 19. Leo akazaliwa mwaka 2013 kisha Sammy akazaliwa mwaka 2015. 
Hazard akiwa na familia yake.Mke na watoto 3.

Picha hisani: jpeg images.

Author: mwanamichezoo blog
E-mail: michezoh@gmail.com


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

The Unknown about Pep Quardiola.

Sergio Ramos afichua makubwa kuhusu Mbappe.