Wanasoka wavuta Bangi.

1.IBRAHIM TANKO.
Raia huyu Wa Ghana, kipenzi cha mashabiki wakinadi  jina lake la utani kama kijana Wa Kumasi,alianza kuonyesha mwanga Wa nyota yake mwaka 2000 akiwa na miaka 17 akiitumikia Borussia Dortmund ya ujerumani.
Baada ya kushiriki mechi ya kombe la ujerumani ( german cup) kati ya Dortmund na Schalke 04,Tanko alipimwa na chembechembe za Tetrahedrocannabinol ambayo ni madini ya bangi zikapatikana kwenye mwili wake.
Alipewa adhabu ya miezi minne aliyokwenda kumalizia Freiburg katika uhamisho. Tanko alistaafu soka akiwa na miaka 30.Tanko akiitumikia Fk Javor ya Serbia.
Picha hisani: Ghanaweb.

2.WILDER MEDINA.
Huyu ni raia Wa Colombia moja kati ya mataifa yenye watukutu na wavunja sheria wengi baada ya bunduki kupatikana kiholela kila eneo la nchi.
Medina akiwa na miaka 18, akiitumikia timu ya ligi divisheni ya pili Rionegro, nchini Colombia, ilikuwa Mara yake ya kwanza kunaswa na uvutaji bangi.
Mwaka 2012 aliendelea na tabia hiyohiyo akiichezea Deported Tolima ambao walitamatisha kandarasi yake na kumtimua.
Wilder Medina.Kwenye picha.
Picha Hisani:JPEG.

3.CHRIS ARMSTRONG.
Ni mchezaji Wa kwanza katika ligi ya premia uingereza kupelekwa katika kambi ya makadirio ya utumizi Wa dawa za kulevya (rehab). Mwaka 1995 akiichezea crystal palace alinaswa na vipimo kwamba alikuwa ametumia Marijuana, kisha akapewa adhabu ya mechi nne.Armstrong kwenye picha.
Picha hisani : JPEG

4.MBULELO MABIZELA.
Mbulelo ni moja kati ya Waafrika wenye bahati kupata uhamisho Wa moja kwa moja kutoka Afrika hadi Uingereza. Mwaka 2003 timu ya Tottenham Hotspurs ilishiriki katika mchuano Wa kirafiki kati yao na Orlando pirates ya Afrika kusini, kisha kocha Wa spurs wakati huo Glenn Noddle akampenda sana Mbulelo Mabizela kwa kiwango chake cha mchezo na kumsajili katika dirisha hilo la usajili.
Alipotua Uingereza hakuwa mwenye bahati sana japo alifunga goli katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Leicester city ,Tottenham wakishinda 2-1,Ila kilichomponza ni kupatikana na utumiaji Wa bangi.
Tatizo la bangi,lilimfanya kurudi Afrika kusini kuichezea Mamelodi Sundowns alipomaliza marufuku ya Miezi 6.
Mabizela akiwa kwenye Uzi Wa spurs ya Uingereza.
Picha Hisani: JPEG.

Author : Mwanamichezoo blog
E-mail: Michezoh@gmail.com.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Maisha ya kutisha ya Eden Hazard.

The Unknown about Pep Quardiola.

Sergio Ramos afichua makubwa kuhusu Mbappe.