"Alinibikiri nikiwa na umri Wa miaka 16,"asema Mkeo Tyson Fury.

BONDIA TYSON FURY NA USHINDI.
Wengi Wa walevi Wa mchezo Wa masumbwi au dondi na kuongeza utukutu ukisema ngumi,wananadi jina tu Tyson Fury kwa kuwa sasa mkanda Wa WBO upo mkononi mwake,baada ya kumparakasa Dentoy wilder katika pambano la tatu mfululizo.
Fury alikuwa ameshiriki mapambano 40 ambapo alikuwa ameshinda 39 na kutoa sare moja kabla ya hili lake na Dentoy wilder,ambalo lilikuwa la tatu.
Fury ameshinda katika pambano ambalo Lilikuwa lenye historia yake, maana ushindi Wa Fury unaamanisha ni trilogy ya kwanza ndani ya miaka 20 ya masumbwi na pili amemcharaza bondia mwenye ngumi nzito zaidi ya mkono Wa kulia.
Pambano hilo lilipiganwa siku ya jumapili tarehe 10/10/21.
Je,Fury ana Mke ? Jibu ni Ndio.

PARIS MULROY FURY.
Mzaliwa huyu Wa Doncaster ndiye anayemlisha Fury vya tumbo na vya ndani hili kupata nguvu za kuwapanguza wapinzani kama vibonzo.

MAISHA.
Fury na Paris walikutana katika Arusi ya kifamilia mwaka 2004,Paris akiwa na miaka 15. Kwa sababu Paris hangeruhusiwa kuwa na uhusiano Wa kimapenzi akiwa na umri huo,Fury alisubiri akafika miaka 16 ndio waanze kuchumbiana. Paris alikuwa mbichi, tunda lake bado kudokolewa na ata ndege Wa angani , kwani Fury alikuwa jamaa la kwanza kumtongoza. 
Baada ya uhusiano Wa miaka mitatu waliamua kufunga pingu za Maisha kama sio jela la ibada.Arusi yao lilikuwa ya kifahari ikifanywa mjini Doncaster mwaka 2008 na kuhudhuriwa na wageni waalikwa 400, katika kanisa la katoliki chains.
Akizungumza katika mahojiano na kituo cha Irish Mirror, Paris alisema Fury alikuwa Wa kwanza kumfunza ya dunia akiwa na umri Wa miaka 16. 

WATOTO.
Watoto Wa Fury na Paris ni 6: Valencia amber,prince afonia amaziah,Athena,Venezuela,prince Tyson Fury II na prince John James.

USHUHUDA MCHEZONI.
Mkewe Fury aliwahi kusema kwamba ni kitu kigumu zaidi kushuhudiwa mumewe katika pambano kinyume na labda ambavyo mashabiki wengi ufikiria. Nikimnukuu  " kila ngumi apigwalo ,nahisi ni kama Mimi  ndio nimepigwa. Kuna wakati watu waliniambia nipo kwenye camera nicheke,nikawauliza nicheke vipi ,wakati mume wangu anapigwa, Ila nifanyeje na ndio mchezo apendao" paris alimueleza mwanahabari Irish mirror.
Paris Fury kwenye picha kubwa kisha kwenye mviringo Fury na Paris. Picha: jpeg.

Author: mwanamichezoo blog
E-mail:michezoh@gmail.com.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Maisha ya kutisha ya Eden Hazard.

The Unknown about Pep Quardiola.

Sergio Ramos afichua makubwa kuhusu Mbappe.