MAYAKA alivyotua kikosini Harambee stars.

Mengi hayajulikani kumhusu kiungo mpya katika timu ya soka taifa la Kenya  Harambee stars,Philip Mayaka aliyeitwa kikosini na kocha Engine Firat,kwa ajili ya kuwavaa Mali ugenini na Uganda katika Mechi za kutafuta nauli ya kushiriki katika mipapurano ya dimba la dunia mwaka 2022 Nchini Qatar.

MAISHA YA SOKA.
Mayaka alipata umaarufu katika shule ya upili st. Anthony kitale katika michezo ya soka la shule za upili yaliyofadhiliwa na cocacola wakati huo.
Mayaka alipoondoka Kenya alielekea zake marekani,alikocheza ndani ya mfumo Wa College ,ambapo timu zinashoriki ligi ya America USL usaka wachezaji.
Sasa ana timu ya Colorado springs.
Mayaka akiwa uwanjani akiitumikia Colorado.
Picha:jpg

KUITWA KATIKA KIKOSI CHA TAIFA.
Akizungumza na wanadijitali wanaosimamia ukurasa wa shirikisho alisema haya nikimnukuu" Sikujua kama naweza kuitwa katika kikosi cha Harambee stars, kwani nacheza katika ligi ya marekani Usl ambayo haina umaarufu.Nilifahamishwa na aliyekuwa mwalimu wangu, mwalimu mkuu Wa shule ya Upili st.Anthony Kitale Cosmas Nabungolo kwamba,kuna afisa Wa Timu ya taifa anayetaka tuongee,wameniita kikosini,wanataka kujua maoni yangu." Mayaka Philip mwenye umri Wa miaka 20.
Kinda huyu aliendelea kuonyesha furaha yake kwa kusema Ni wakati naye aishughulikie familia yake.

 Mwandishi
Mwanamichezoo blog
E-mail: Michezoh@gmail.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Maisha ya kutisha ya Eden Hazard.

The Unknown about Pep Quardiola.

Sergio Ramos afichua makubwa kuhusu Mbappe.