Mshambulizi pekee anayemvuruga Virgil Van Dijk

VIRGIL KWA ERLING HAALAND.
Beki kati Wa Liverpool na taifa la Uholanzi, Virgil Van dijk amemsifia mshambuliaji wa Borussia Dortmund  Erling Haaland, kwa kusema Ni moja ya mastaa Wa sasa walio na kila kiungo kumbabaisha beki mzuri duniani.
"Haaland ni straika wa kipekee kwani ana nguvu,ana mbio na kila kiungo cha kumsababishia beki maisha magumu," Virgil akizungumza na Sky sports.
Mwamba huyu Wa Netherlands ameongeza kwamba ,muundo wake Wa kucheza Ni kama ule Wa James Jamie Vardy Wa Uingereza na Leicester. "Ana nguvu zaidi ya vardy ila mchezo wao Ni mmoja" dijk akaongeza.
Kwenye picha Ni Virgil na erling wakipunga mkono baada ya mechi ya Netherlands dhidi ya Norway.
PICHA:GETTY IMAGES.

KUTUA ANFIELD.
Mshambulizi huyu amehusishwa pakubwa na wekundu Wa An field akitajwa kama mrithi Wa Takumi minamino na Firmino ambao kiwango chao sio cha magoli kila Mara.
Baada ya Virgil kumtilia shombo nyota huyu akisema Ni moja kati ya washambulizi walionitatiza,uenda hili likapandisha homa ya Liverpool kumnyakua katika dirisha la uhamisho lijalo. Dau lake sokoni Ni  £68million.

Mwandishi
Mwanamichezoo blog
E-mail: Michezoh@gmail.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Maisha ya kutisha ya Eden Hazard.

The Unknown about Pep Quardiola.

Sergio Ramos afichua makubwa kuhusu Mbappe.