Beti tano Motomoto

Ni wikendi ya kimichezo,ambapo michezo mbalimbali inatakatwa. Mwanamichezo blog inakupakulia tano za Leo.

UFARANSA .LIGUE 1 
PSG dhidi ya Rennes.
Mechi hii ni kubwa sana katika uwanja Wa PARC de princes nyumbani mwa Psg.
PSG
 Mabwenyenye Wa Paris katika mechi 5 zilizopita hawajafunga magoli zaidi ya matatu.Katika mechi 6 za ligi hawajashindwa. Jumlisha mechi mbili za klabu bingwa barani uropa.
RENNES
Katika mechi 6 za ligue 1 wamepoteza mchezo mmoja pekee.Katika 5 walizoshinda hakuna magoli zaidi ya matatu.
UBASHIRI 
Psg kushinda.
Magoli chini ya 3.

UINGEREZA .EPL
CRYSTAL PALACE DHIDI YA LEICESTER
CRYSTAL PALACE
Palace hawajapoteza mchezo wowote wakiwa nyumbani chini ya kocha Patrick Vieira. Michezo miwili waliyopoteza in dhidi ya Liverpool na Chelsea.Mechi ya juzi wametoa sare dhidi ya Brighton.
LEICESTER
Vijana Wa kocha Brendan Rodgers hawana msururu mzuri Wa matokeo baada ya kupiga Manchester city katika pambano LA kombe la community shield.
Wameshinda mechi moja dhidi ya Wolves katika michezo 6 ya ligi.
UBASHIRI
crystal palace kushinda au sare.

 SPAIN .LALIGA.
ESPANYOL dhidi ya REAL MADRID.
ESPANYOL
Wameshinda mechi moja kati ya saba za ligi. Katika Mechi nne za ligi hawana goli ata moja.
REAL MADRID.
wanakuja katika mchezo na jeraha LA kupigwa na sheriff transpol ya Moldova katika pambano la klabu bingwa barani ulaya,2-1.
Kikosi cha Carlo Ancelloti hakijashindwa katika mechi saba za laliga.
UBASHIRI
Real Madrid kushinda.

ITALIA SERIA A
ROMA DHIDI YA EMPOLI
ROMA
Kikosi cha kocha Jose Mourinho kinaonekana kuwa katika ubora wake,wakati pia mshambulizi Tammy Abraham anafanya kweli katika kikosi hicho.Roma wanafunga zaidi ya magoli 2 katika kila mechi.
EMPOLI.
Empoli baada ya kupandishwa ngazi wamecharuka kiukweli katika eneo la ufungaji. Wamefunga goli katika kila mechi waliocheza isipokuwa mechi moja tu.
UBASHIRI
Roma kushinda .Magoli zaidi ya mawili katika mechi hio.

UJERUMANI. BUNDESLIGA.
BAYERN MUNICH DHIDI YA EINTRANCH FRANKFURT .
BAYERN MUNICH.
Bayern kila Mara wanapomkuta Frankfurt wanamlisha magoli zaidi ya matatu. Katika mechi ya majuzi alimpa 5-0. Bayern wakianza kufunga wanasimamishwa na kipenga cha mwamuzi.Wametoka kuipiga Dynamo Kiev klabu bingwa barani ulaya.
EINTRANCH Frankfurt
Hawana bahati wapatano na wakali hawa Wa bundesliga. Hawana historia katika uwanja Wa Allianz arena kwa sasa.
UBASHIRI.
Bayern Munich kushinda. Magoli zaidi ya 3.
@mwanamichezo arts.

Mwandishi.
Mwanamichezo blog.
E-mail : Michezoh@gmail.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Maisha ya kutisha ya Eden Hazard.

The Unknown about Pep Quardiola.

Sergio Ramos afichua makubwa kuhusu Mbappe.