Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2020

UKOCHA HARAMBEE STARS.

Imekuwa ni kama sinema isiyo na mfawidhi katika maegeuzi yaliyofanyika katika uongozi Wa timu ya taifa soka harambee stars. Kocha Francis kimanzi anayesemwa na wengi kama kocha aliyewahi kuwa na mafanikio makubwa sana katika kibarua chake baada kuipandisha ngazi stars katika msimamo Wa shirikisho LA soka duniani FIFA kutoka nafasi ya 104 hadi 67. Lakini binadamu ata umpe ghorofa atataka kuishi mawinguni. Hilo sio tatizo, kocha mpya mwanahabari Jacob Ghost Mulee amechukua hatamu za uongozi katika mkataba Wa miaka mitatu. Kuna atiati kwamba kimanzi kanyofolewa baada ya kuingia katika himaya ya uongozi Wa shirikisho LA kandanda humu nchini FKF. Yote Tisa kumi ni kwamba hauwezi kushuka kutoka kwa ndege uliyoabiri kisa na maana rubani kabadilishwa. Mulee ambaye vilevile anamiminiwa sifa kedekede anahitaji uungwaji  mkono kutoka kwa kila mzalendo.

LEO MICHEZONI

Uenda klabu cha arsenal  kikakumbwa na matatizo hii Leo katika mchezo wao dhidi ya rapid Wien katika kampeni za kombe LA ligi bara uropa. Hii ni baada ya ujumbe Wa kiungo Wa kati mjerumani mesut ozil akikashifu kuachwa kwake nje ya kikosi .Baadhi ya wachezaji Wa timu hii wameonekana kupendezwa na ujumbe wake.